Kikosi chetu kesho mchana kinarejea nchini kutoka Morocco baada ya kambi ya wiki tatu ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi 2021/22.
Timu itaondoka Morocco leo jioni na ikifika nchini moja kwa moja inaingia kambini kujiandaa na Tamasha kubwa la kihistoria la Simba Day.
Ikiwa nchini Morocco, Simba imecheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya FA Rabat na Olympique Club Khouribga ambazo zote ziliisha kwa sare.
Advertisement
Kikosi kitaendelea kujifua hapa nchini baada ya kurejea kutoka Morocco hadi msimu mpya wa ligi utakapoanza.
Tunatarajia kucheza mechi kadhaa za kirafiki za ndani kama taratibu zilizopangwa zitakamilika.