Kikosi chetu leo jioni kimetoka sare ya bila kufungana katika mechi ya kirafiki dhidi ya Coastal Union mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Arusha International School jijini Arusha.
Mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu 2021/22.
Mchezo wa leo ni wa kwanza wa kirafiki ikiwa ni siku nne tangu kikosi kilipowasili jijini hapa kwa kambi ya wiki mbili.
Katika mchezo huo timu zote zilishambuliana kwa zamu na kutengeneza mashambulizi kadhaa lakini idara za ulinzi zilikuwa makini kuondoa hatari.
Kiungo wetu Bernard Morrison alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 37 baada ya kumlipizia mchezaji wa Coastal kutokana na kufanyiwa madhambi.
Benchi la ufundi chini ya Kocha Didier Gomes limedhika na viwango vya wachezaji walivyoonyesha na lina imani kubwa tunaenda kufanya vizuri kwenye michuano yote msimu mpya wa ligi.
Kocha Gomes aliwatoa Kakolanya, Gadiel, Wawa, Mkude, Bwalya, Dilunga, Mugalu na Sakho na kuwaingiza Ally Salum, Kennedy Juma, Henock Inonga, Abdulsamad, Sadio Kanoute na Duncan Nyoni.
Kikosi kamili kilichocheza mechi hiyo;
Benno Kakolanya, Bernard Morrison, Gadiel Michael, Joash Onyango, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Hassan Dilunga, Rally Bwalya, Yusuph Mhilu, Pape Ousmane Sakho na Ibrahim Ajibu.