Simba Sports Club
Pre Season Arusha

Nyoni aongoza Stars kwenye ushindi

7 Sep 2021

Mchezaji wetu Erasto Nyoni amekuwa mmoja wa wachezaji wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) waliofunga katika ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Madagascar uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Katika mchezo huo wa kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka 2022, magoli mengine yalifungwa na Novatus Dickson na Feisal Salum.

Advertisement

Kwa ushindi huo, Tanzania sasa inaongoza katika msimamo wa kundi lao lenye timu za DR Congo, Benin na Madagascar.

Wachezaji wengine wa Simba waliocheza katika mchezo huo walikuwa ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein na Muzamiru Yassin

Back to homepage
Share this story