Simba Sports Club
Simba Day 2021

Kanoute kuanza, Mugalu kuongoza mashambulizi dhidi ya Mazembe

19 Sep 2021

Kiungo mpya Saido Kanoute na mshambuliaji Kibu wataanza katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya TP Mazembe utakaoanza saa 11 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Nyota huyo ataonekana kwa mara ya kwanza mbele ya mashabiki wetu ambao wameujaza uwanja mzima wa Mkapa.

Mshambuliaji Chris Mugalu ataongoza mashambulizi huku kiungo fundi Rally Bwalya akimsaidia kwa ukaribu.

Walinzi wa kati Joash Onyango na Pascal Wawa wataendelea kusimama pamoja juu yao akiwepo Taddeo Lwanga kama kawaida.

Advertisement

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Pascal Wawa (6), Thadeo Lwanga (4) Bernard Morisson (3) Sadio Kanoute (13), Chris Mugalu (7)

Rally Bwalya (8), Denis Kibu (38)

Wachezaji Wa Akiba- Beno Kakolanya, Ally Salim, Jeremiah Kisubi, Feruzi Teru, Kennedy Juma, Erasto Nyoni, Gadiel Michael Henonga Baka, Israel Mwenda, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin. Pape Sakho, Duncan Nyoni, Abdulasammad Ally, Hassan Dilunga, Peter Banda,Ibrahim Ajib, Medie Kagere, John Bocco,

Back to homepage
Share this story