Ndemla kuanza, Bocco, Kagere kuongoza mashambulizi dhidi ya Azam leo

Kocha Didier Gomes amemuanzisha kiungo Said Ndemla katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC utakaopigwa katika Uwanja wa Azam Complex saa moja usiku.

Katika mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union tuliopata ushindi wa mabao 2-0, Ndemla alitokea benchi lakini leo Kocha Gomes ameamua kumpa nafasi ya kuanza.

Katika eneo la kiungo wa ulinzi Ndemla atacheza sambamba na Taddeo Lwanga na Mzamiru Yassin kutokana na aina ya mchezo wenyewe.

Nahodha John Bocco na Medie Kagere wataongoza safu ya ushambuliaji wakisaidiwa na Hassan Dilunga kutoka upande wa kushoto.

Mlinda mlango Beno Kakolanya walinzi wa pembeni David Kameta ‘Duchu’ na Gadiel Michael wameendelea kupata nafasi kama ilivyokuwa mchezo uliopita.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Beno Kakolanya (30), David Kameta (27), Gadiel Michael (2), Joash Onyango (16), Kennedy Juma (26), Taddeo Lwanga (4), Mzamiru Yassin (19), Said Ndemla (13), Medie Kagere (14), John Bocco (22), Hassan Dilunga (24).

Wachezaji wa Akiba: Ally Salim (1), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Ibrahim Ame (5), Erasto Nyoni (18), Chris Mugalu (7), Rally Bwalya (8).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER