Viungo wetu wakabaji Mzamiru Yassin na Sadio Kanoute hawatakuwa sehemu ya mchezo wetu wa kesho wa Ligi ya NBC dhidi ya Namungo FC utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa kutokana na kuendelea kuuguza majeraha.
Nyota hao walipata maumivu katika mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union ambapo walishindwa kuendelea na mechi muda mfupi kabla ya kwenda mapumziko.
Daktari wa timu, Yassin Gembe amesema wachezaji hao hawakupata majeraha makubwa lakini wataukosa mchezo wa kesho ili kuwakinga wasiumie zaidi na kuwapa nafasi ya kupona vizuri.
“Mzamiru na Kanoute hawakupata majeraha makubwa ila tumewapumzisha ili kuwakinga wasijitoneshe, katika mchezo unaokuja nadhani watakuwa wamerejea uwanjani,” amesema Dk. Gembe.
3 Responses
Pambanieni Timu .. mcheze kwa kutulia sio papara, Ajibu na Sakho warudi kikosini
Ushindi ni wetu, furaha ni yetu, huzuni ya muda mfupi haitukatishi tamaa na ubingwa wa tano mfululizo ni wetu.
All the best MNYAMA
Hakika ni kwa wachezaji kucheza kwa utulivu wasiwe na hofu ushindi utapatikana tu.