Mwanzo mzuri Kombe la Shirikisho

Kikosi chetu kimeanza vizuri Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya makundi baada ya kuichakaza ASEC Mimosas mabao 3-1 mchezo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Pape Sakho alitupatia bao la kwanza kwa ‘tiktak’ dakika ya 12 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Shomari Kapombe.

Dakika 10 baadaye tulifanya shambulizi kali langoni mwa ASEC ambapo alimanusura Medie Kagere atuandikie bao la pili lakini shuti lake likagonga mwamba wa chini.

Dakika ya 45, Peter Banda alipoteza nafasi ya wazi baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mohamed Hussein na kumpiga chenga mlinda mlango wa ASEC kabla ya shuti lake kupaa juu.

Dakika ya 59 ASEC walisawazisha bao hilo kupitia kwa Ki Aziz kwa shuti la mguu wa kushoto baada ya walinzi wetu kuzembea kuondoa hatari.

Shomari Kapombe alitupatia bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 78 baada ya Yusuf Mhilu kufanyiwa madhambi na mlinda mlango wa ASEC.

Dakika moja baadaye Banda alitufungia bao la tatu akimaliza mpira wa krosi uliopigwa na Nahodha John Bocco.

Kocha Pablo aliwatoa Sakho, Kagere, Sadio Kanoute, Banda na Bwalya kuwaingiza Mzamiru Yassin, John Bocco, Yusuf Mhilu, Erasto Nyoni na Israel Patrick.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER