Mo, Africarriers, waungana na Watanzania kuwamaliza Uganda Kesho

Rais wa heshima wa Klabu, Mohamed Dewji ‘Mo’ amenunua tiketi 5000 kwa ajili ya mashabiki kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa maruadiano wa kufuzu fainali za Afrika (AFCON) dhidi ya Uganda utakaopigwa kesho saa mbili usiku.

Mo ameungana na Watanzania wengine ambao wamenunua tiketi kwa ajili ya kutoa hamasa kwa Taifa Stars ili kupata ushindi kesho na hatimaye tujiweke katika nafasi ya kufuzu fainali hizo.

Wadhamini wetu Africarriers nao wamenunua tiketi 2000 kuchangia hamasa kuelekea mchezo wa kesho kwakuwa hili ni suala la kitaifa.

Juzi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’ nae amechangia tiketi 500 huku Mwenyekiti wa klabu Murtaza Mangungu nae akichangia tiketi 600.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER