Mgunda: Ushindi huu wetu sote

Kocha Mkuu Juma Mgunda amesema ushindi wa mabao 4-0 tuliopata dhidi ya Ruvu Shooting ni wetu sote benchi la ufundi, wachezaji pamoja na mashabiki.

Mgunda amesema kila mmoja kwa nafasi yake ametimiza majukumu yake kwa ufasaha na hilo ndilo lililosababisha ushindi huo mnono ulioleta furaha kwa Wanasimba.

Akizungumzia mchezo wenyewe Mgunda amewasifu wachezaji kwa kazi kubwa waliofanya na kufuata vizuri maelekezo waliyopewa.

“Namshukuru Mungu tumefanikiwa kupata ushindi mnono, huu umetokana na mshikamano kutoka kwa benchi la ufundi, wachezaji na mashabiki waliokuja kutupa sapoti,” amesema Mgunda.

Mgunda amesisitiza kuwa kwenye mpira wa miguu kuna kipindi unakuwa bora na wakati mwingine inakuwa tofauti kwa hiyo mashabiki wanapaswa kukubali nyakati zote.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER