Mgunda: Tupo Tayari Kupambana na Polisi kesho

Kocha Mkuu Juma Mgunda, amesema kikosi kiko tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Uwanja wa Ushirika saa 10 jioni.

Mgunda amesema maandalizi ya mchezo yamekamilika na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri kwa ajili ya kuhakikisha tunapambana kutafuta alama tatu.

Mgunda ameweka wazi kuwa mchezo utakuwa mgumu na tutaingia uwanjani kwa kuiheshimu Polisi na hatutaidharau licha ya nafasi waliyopo kwenye msimamo wa ligi.

“Maandalizi ya mchezo yamekamilika na wachezaji wapo kwenye hali nzuri, tunajua mechi itakuwa ngumu. Ingawa Polisi haipo kwenye nafasi nzuri lakini tutaiheshimu lengo letu ni kupata pointi tatu,” amesema Mgunda.

Mgunda ameongeza kuwa wachezaji wote 22 waliosafiri wako vizuri na tunaendelea kuwaombea waamke salama kesho watuwakilishe kwa kutupa furaha.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER