Mgunda: Tunarudi kumalizia kwa Mkapa

Kocha Mkuu Juma Mgunda, amesema licha ya kupata ushindi mnono ugenini lakini kazi bado hatujamliza tunarudi nyumbani kujipanga kwa ajili ya mechi ya marudiano.

Mgunda amesema mchezo wa marudiano hautakuwa rahisi licha ya mtaji mzuri wa mabao na hatutawadharau Premiero De Agosto badala yake tutajipanga kuhakikisha tunashinda.

Mgunda ameongeza kuwa kwa sasa bado mshikamano kwa Wanasimba unahitajika ili kutimiza malengo yetu tuliyojiwekea kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Tunamshukuru Mungu tumepata ushindi mnono ugenini lakini hii haimaniishi tumemaliza kazi hapana. Hii ni mechi ya kwanza kuna nyingine tutacheza nyumbani.

“De Agosto sio timu mbaya ni mabingwa wa Angola pamoja na ushindi wa leo lakini bado hatujafuzu, tunarudi nyumbani kujipanga kwa ajili ya mchezo wa marudiano,” amesema Mgunda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER