Mgunda: Maandalizi ya De Agosto yamekamilika asilimia 80

Kocha Mkuu Juma Mgunda, amesema maandalizi ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Premiero De Agosto kutoka Angola utakaopigwa Jumapili katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, yamekamilika kwa asilimia 80.

Mgunda amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri wakiwa na ari tayari kuipigania timu kuwapa furaha Wanasimba na Watanzania kwa ujumla.

Mgunda ameongeza kuwa tunakwenda kukutana na timu ambayo tumeiona na tunaijua hivyo tunajiandaa kuhakikisha tunatumia vizuri mapungufu yao kupata ushindi nyumbani.

“Naweza kusema maandalizi yamekamilika kwa asilimia 80, wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri kuhakikisha wanatetea bendera ya taifa na kuwapa furaha Wanasimba,” amesema Mgunda.

Mgunda amesema katika mchezo wa Jumapili tutaendelea kukosa huduma ya mlinzi wa kulia Shomari Kapombe ambaye anaendelea kupona majeraha yake na Jimmyson Mwanuke.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER