Mgunda, Chama wakabidhiwa tuzo za Desemba

 

Kocha Msaidizi Juma Mgunda na kiungo mshambuliaji Clatous Chama, wamekabidhiwa tuzo zao Ligi Kuu ya NBC za mwezi Desemba.

Mgunda ameshinda tuzo hiyo kwa kuwapiku Hans Van Plujim wa Singida Big Stars na Nasreddine Al Nabi wa Yanga ambao aliingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.

Kwa upande wake Chama aliwashinda Nahodha John Bocco na Fiston Mayele wa Yanga.

Mgunda na Chama wamekabidhiwa kila mmoja tuzo, mfano wa hundi na Sh 1,000,000 na Kisimbuzi cha Azam TV.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER