Mgunda awapongeza wachezaji ushindi wa Prisons

 

Kocha Mkuu Juma Mgunda amewapongeza wachezaji kwa kuonyesha kiwango safi katika ushindi wa mabao 7-1 tuliopata dhidi ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wa ligi kuu uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mgunda amesema wachezaji wamejitahidi kufuata maelekezo hasa kipindi cha pili na ndicho kilichotusaidia kupata ushindi huo mnono wa kufungia mwaka 2022.

Akizungumzia kiwango cha nyota mpya Said Ntibazonkiza, Mgunda amesema ni mchezaji mzuri na uzoefu wake utasaidia katika kikosi.

“Baada ya mlinzi Henock Inonga kuumia wachezaji wenzake waliingia unyonge wakawa hawako vizuri, kipindi cha pili tuliwajenga kisaikolojia na walivyorudi wakafanya vizuri nawashukuru kwa kufuata maelekezo kwa usahihi na kutupatia ushindi mnono.

“Ntibazonkiza ni mchezaji mzuri tunaamini uzoefu wake utatusaidia na ndiyo maana tukamsajili,” amesema Mgunda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER