Mchezo dhidi ya Polisi kupigwa Jumatano Chamazi

Bodi ya Ligi imetangaza mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Polisi Tanzania utapigwa Jumatano Mei 24, saa moja usiku katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Mchezo huo ulisogezwa mbele kipindi ambacho tulikuwa tunashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ili kutupa nafasi ya maandalizi mazuri.

Baada ya kusogezwa mbele ulikuwa haujapangiwa tarehe ya kuchezwa lakini leo Bodi ya Ligi imeweka hadharani kila kitu.

Pia mchezo wetu wa mwisho wa kufungia msimu wa Ligi Kuu ya NBC 2022/23 dhidi ya Coastal Union utapigwa Mei 28 katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Kikosi kinaendelea na mazoezi chini ya kocha mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ na wasaidizi wake.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER