Mchezo dhidi ya Dodoma kesho kupigwa jioni

Mechi yetu ya kesho ya Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji ambayo awali ilikuwa ichezwe saa moja usiku sasa itapigwa saa 10 jioni.

Tayari uongozi wa klabu umepokea taarifa ya maandishi kutoka Bodi ya Ligi kuhusu mabadiliko hayo ya muda wa mchezo.

Maandalizi ya mchezo yanaendelea vizuri kila kitu kipo kama kilivyopangwa na kinachosubiriwa ni muda tu ufike mchezo huo upigwe hapo kesho.

Viingilio vya mchezo huo vipo kama ifuatavyo:

VIP A Sh 15,000
VIP B na C Sh 10,000
Mzunguko Sh 5000

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER