Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Jenerali Seyni Kounteche ikiwa ni maandalizi kabla ya kushuka dimbani kuikabili US Gendarmerie Nationale katika mchezo wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika kesho.
Mazoezi hayo yamefanyika saa 11 Jioni kwa saa za Niger muda ambao mchezo wetu wa kesho utachezwa na saa moja usiku kwa saa za nyumbani.
Katika mazoezi hayo wachezaji wameonekana kuwa na ari na morali na kuonyesha jitihada ili kulishawishi benchi la ufundi kuwapa nafasi.
Uwanja wa Jenerali Seyni Kounteche unatumia nyasi asilia na una uwezo wa kuingiza mashabiki 35,000 lakini kwenye mchezo wa kesho wenyeji Gendarmerie wameruhusiwa kuingiza mashabiki 1,000 pekee.
One Response