Matola afunguka ukame wa mabao

Kocha Msaidizi Seleman Matola, ameweka wazi kuwa suala la ukame wa mabao linaendelea kufanyiwa kazi mazoezini na matunda yake huenda yakaanza kuonekana kesho katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mbeya Kwanza.

Matola amesema changamoto ya kukosa mabao imekuwa ikiendelea lakini tiba yake imeanza kupatikana na tunategemea katika matokeo yatapatikana kuanzia kesho.

Akizungumzia mchezo wa kesho, Matola amesema hautakuwa rahisi sababu Mbeya Kwanza ni timu nzuri lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

“Ni kweli suala la ukame wa mabao ni kubwa kikosini hata sisi tumeliona, tunalifanyia sana kazi mazoezini na kuanzia mchezo wetu wa kesho dhidi ya Mbeya Kwanza matunda yataanza kuonekana.

“Mchezo utakuwa mgumu, Mbeya Kwanza ni timu nzuri na ligi imefikia pagumu lakini na sisi tunazihitaji pointi tatu na maandalizi yote yamekamilika,” amesema Matola.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER