Mangungu: Tumefanya mambo makubwa Simba

Mwenyekiti wa klabu, Murtaza Mungungu amesema Uongozi wa klabu umefanya mambo mengi ya mendeleo kwa timu na yanayonekana.

Mangungu ameyasema hayo katika Mkutano Mkuu wa Wanachama uliofanyika katika Ukumbi wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Mangungu amesema katika uongozi umesimamia fedha zilizochangishwa na wanachama pamoja na mashabiki kwa ajili ya kujenga uzio katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena na zimetumika kama ilivyokusudiwa.

Mangungu ameongeza kuwa watu wanabeza uwekezaji lakini wamesahau kuwa kabla klabu ilikuwa inaingiza mapato bilioni 1.6 lakini sasa inaingiza bilioni 6.9 kwa mwaka.

“Uongozi tumefanya mambo mengi makubwa, tumeweza kusimamia vema pesa zilizochangwa na wanachama kwa ajili ya kujenga uzio katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena na tayari tumefanya hivyo na kiasi kilichobaki tuliongezea katika gharama ya kambi,” amesema Mangungu.

Aidha Mangungu amesema hata kukosolewa hawakatai lakini inatakiwa iwe kwa stara na sio matusi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER