Murtaza Mangungu amefanikiwa kutetea kiti chake baada ya kuchaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa klabu kwa muda wa miaka minne katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika jana.
Mangungu ametetea nafasi yake baada ya kumshinda Adv. Moses Kaluwa kwa kura 1311 dhidi ya 1045 alizopata mpinzani wake.
Matokeo ya Uchaguzi huu yamechelewa kutangazwa kutokana na zoezi la uhesabiaji kuchukua muda mrefu kutokana na idadi kubwa ya wanachama waliojitokeza kupiga kura.
Kwa mara ya kwanza Mangungu alichaguliwa Mwenyekiti wa klabu miaka miwili iliyopita akichukua nafasi ya Swedi Mkwabi aliyejiuzulu nafasi hiyo.
Idadi ya kura 2363 Kura halali 2356
Kwa upande wa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi walioshinda ni
- Dr Seif Ramadhan Muba 1636
- Asha Baraka 1564
- CPA Issa Masoud Iddi 1285
- Rodney Chiduo 1267
- Seleman Harubu 1250