Makamu wa Rais atupongeza kwa kutangaza Utalii wa Zanzibar

Makamu wa pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hemed Suleiman Abbullah ameupogeza uongozi wa Klabu kwa kuamua kutangaza Utalii wa Zanzibar kupitia michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Mh. Abdullah amesema tumefanya jambo zuri kutangaza Utalii kwakuwa ni timu kubwa na ina wafuasi wengi hivyo tunafika sehemu kubwa duniani.

“Kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar naupongeza Uongozi wa Simba kwa kuamua kutangaza Utalii wetu, hili ni jambo kubwa mmefanya na mnastahili pongezi,”amesema Mh. Abdullah.

Kwa upande wake Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amemueleza Mh. Abdullah kuwa mipango yetu ni kutumia michuano ya Mapinduzi kusaidia kukuza uchumi kupitia kutangaza Utalii.

“Simba ni Klabu kubwa na tuna wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii tumeona kupitia michuano hii itakuwa fursa kwetu kuutangaza Utalii na tunafahamu ndio chanzo kikuu cha pato la taifa hili,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER