Kocha Msaidizi, Seleman Matola amesema maandalizi ya mchezo wa kesho wa fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Mlandege yamekamilika.
Matola amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na hakuna ambaye tutamkosa kutokana nakuwa majeruhi au kutumikia adhabu ya kadi.
Matola ameongeza kuwa utakuwa mchezo mgumu na hatutaingia kwa kuidharau Mlandege kwakuwa lengo letu ni kuchukua ubingwa wa michuano hii.
“Kikosi chetu kipo kwenye hali nzuri wachezaji wapo timamu kimwili na kiakili kwa ajili ya mchezo wa kesho.
“Haitakuwa mechi nyepesi na tunaiheshimu Mlandege lakini tumejipanga kuwakabili na lengo letu ni kuchukua taji,” amesema Matola.
Akizungumzia kwa niaba ya wachezaji mlinda mlango, Ally Salim amesema wapo tayari kupambana kuhakikisha timu inapata ushindi na kuchukua ubingwa.
“Ukifika hatua hii hakuna mechi nyepesi, Mlandege ni timu nzuri ndio maana imefika fainali lakini nasi tumejipanga na tupo tayari kupambana ili kuibuka na ubingwa,” amesema Ally.