Wadhamini wakuu wa klabu, Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-bet imetupa pesa taslimu Sh. 100,000,000 baada ya kufanikiwa kuingia Robo Fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.
Pesa hiyo ni bonus kwa mujibu wa mkataba ambapo tukifanikiwa kuingia hatua hiyo M-bet kama wadhamini wakuu wanapaswa kutoa kitita hicho.
Meneja Masoko wa M-bet, Alan Mushi amesema wanajivunia kufanya kazi nasi na uwepo wao kwetu unaendelea kutufanya kuwa imara zaidi na kupata mafanikio makubwa.
“M-bet inakabidhi hundi ya Sh. 100,000,000 kwa Simba kwa kufanikiwa kuingia Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni bonus kwa mujibu wa mkataba. M-bet tunajivunia kufanya kazi na Simba na tunaamini uwepo wetu utawafanya kupata mafanikio zaidi,” amesema Mushi.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula amewashukuru M-bet kwa kutimiza makubaliano kwa mujibu wa mkataba.
“Mpira wa miguu unahitaji uwekezaji mkubwa na M-bet mmefanya jambo zuri kiasi hiki kimetuongezea hamasa,” amesema Kajula.