Lengo lilikuwa kufuzu ugenini…

Wakati timu inaondoka kuelekea Benin kwa ajili ya mchezo wetu wa tano hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas, tulikuwa na lengo la kufuzu robo fainali tukiwa ugenini ili kuweka historia ingawa imeshindikana.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kutoka nchini Benin ambapo amesisitiza tutautumia vema uwanja wa nyumbani kuhakikisha tunashinda mechi ijayo.

Ahmed amesema tunahitaji ushindi wowote dhidi ya US Gendarmerie katika mchezo wetu wa mwisho utakaopigiwa Benjamin Mkapa, Aprili 3 saa moja usiku ili kufuzu robo fainali ya michuano hiyo bila kujali matokeo ya mechi ya RS Berkane na ASEC.

Ahmed amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani siku hiyo kuipa sapoti timu kusaidia kutinga robo fainali ambapo amesema tumepeleka maombi CAF ya kuruhusu idadi kubwa zaidi ya 35,000 inayotolewa mara zote.

“Tumepoteza mchezo lakini hatujapoteza lengo la kutinga robo fainali. Awali tulipanga kufuzu tukiwa ugenini na kuweka historia lakini imeshindikana, tumerudi nyumbani kujipanga na mchezo wa mwisho dhidi ya Gendarmerie.

“Tiketi yetu ya kuingia robo fainali tunayo wenyewe, tunahitaji kushinda tu mchezo wetu bila kuangalia matokeo ya mechi nyingine ndiyo maana nasisitiza mashabiki wajitokeze kwa wingi Aprili 3 kwa Mkapa kusapoti timu yao,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER