Kwa heri Ibrahim Ajibu

Uongozi wa klabu umefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajibu baada ya kuangalia faida za pande zote.

Ajibu ni mchezaji kijana mwenye uwezo mkubwa lakini hakupata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwa hiyo ili kulinda kipaji chake tumekubali kumruhusu kwenda kutafuta timu itakayompa nafasi.

Kipaji cha Ajibu kilionekana akiwa katika timu yetu ya vijana ya Simba B kabla ya kupandishwa kwa wakubwa ambapo pia alionyesha uwezo mkubwa.

Simba inamtakia kila la heri Ajibu katika maisha yake mapya ya soka nje ya Simba ni matumaini yetu ataendelea kuonyesha uwezo wake kwa kuwa ana kipaji kikubwa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER