Kuziona Simba, Al Hilal Buku Mbili

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally ametangaza viingilio vya mchezo wetu kirafiki wa kimataifa dhidi ya Al Hilal utakaopigwa kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni ambapo cha chini kitakuwa Sh. 2000.

Ahmed amesema viingilio hivyo vinatokana na jana kucheza mechi ya Ligi na watu wamelipa hivyo ili kuwapunguzia majukumu tumeweka kiingilio kidogo ambacho kila mtu atakimudu.

Ahmed ameongeza kuwa kesho itakuwa siku ya mtoko wa mwisho wa wiki kwahiyo Wanasimba wanapaswa kuja uwanjani kufurahi na familia ambapo watoto chini ya umri wa miaka 10 wataingia bure.

“Jana tumecheza mechi mashabiki walikuja kwa wingi uwanjani. Haitakuwa vizuri kuweka viingilio vikubwa badala yake tunafanya kama mtoko ili Wanasimba waje kwa wingi na familia zao,” amesema Ahmed.

Viingilio vilivyopangwa

VIP A Sh. 10,000
VIP B Sh. 5000
Mzunguko 2000

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER