Kocha Gomes afanya mabadiliko kikosi dhidi ya Mbeya City leo

Baada ya kuwakosa baadhi ya wachezaji, Kocha Didier Gomes amefanya mabadiliko kadhaa ya kikosi kitakachoshuka dimbani kuikabili Mbeya City kwenye mchezo wa leo wa ligi kuu utakaofanyika leo saa moja usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mlinda mlango Beno Kakolanya atachukua nafasi ya Aishi Manula ambaye anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Mlinzi Kennedy Juma leo amepangwa kucheza nafasi ya kiungo mkabaji kuchukua mikoba ya Taddeo Lwanga ambaye naye anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Erasto Nyoni nae amepangwa kucheza namba nane akisaidiana na Kennedy kwenye kukaba wakati Bernard Morrison akianza kama winga wa kulia.

Nahodha John Bocco ataendelea kuongoza mashambulizi akisaidiana na Luis Miquissone, Rally Bwalya na Morrison.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Beno Kakolanya (30), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Pascal Wawa (6), Kennedy Juma (26), Bernard Morrison (3), Erasto Nyoni (18), John Bocco (22), Rally Bwalya (8), Luis Miquissone (11).

Wachezaji wa Akiba: Ally Salim (1), Gadiel Michael (2), Mzamiru Yassin (19), Hassan Dilunga (24), Clatous Chama (17), Medie Kagere (14), Miraji Athumani (21)

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER