Timu yetu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ leo usiku itakuwa na mchezo muhimu wa kufuzu michuano ya Afrika AFCON dhidi ya Algeria utakaopigwa katika Uwanja wa Mei 19 nchini Algeria.
Taifa Stars inahitaji alama moja tu ili kupata tiketi ya kufuzu fainali hizo ambazo zitafanyika mwakani nchini Ivory Coast.
Stars ipo kundi F ikiwa na alama saba ambapo kama tutapata alama moja tutakuwa tumefuzu kwakuwa wapinzani wetu Uganda hawatazifikia hata kama wakishinda leo dhidi ya Niger.
Uongozi wa klabu upo pamoja na Watanzania wote kuitakia kheri Stars kufanya vizuri ili tufuzu michuano hii mwakani.
Simba tunawatakia kheri wachezaji wetu, Kennedy Juma, Mzamiru Yassin, John Bocco na Kibu Denis mchezo mwema na waisaidie Stars kuhakikisha tunashinda.
Kama tutafanikiwa kupata alama moja leo Tanzania tutakuwa tumefuzu fainali za Afrika kwa mara ya tatu baada ya mwaka 1980 na 2019.