Kikosi Kitakachotuwakilisha dhidi ya Yanga leo

Mshambuliaji kinara Moses Phiri amepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya watani wetu Yanga utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11 jioni.

Kama kawaida Phiri atapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Clatous Chama, Pape Sakho na Augustine Okrah.

Mchezaji mwandamizi Jonas Mkude ataongoza safu ya kiungo wa ulinzi ambapo atacheza sambamba na Mzamiru Yassin.

Kikosi kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Israel Patrick (5), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Pape Sakho (10), Mzamiru Yassin (19), Moses Phiri (25), Clatous Chama (17), Augustine Okrah (27).

Wachezaji wa akiba

Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Nassor Kapama (35), Peter Banda (11), John Bocco (22), Habibu Kyombo (32), Kibu Denis (38).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER