Leo saa moja usiku katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kikosi chetu kitaikabili Vipers kwenye mchezo wa nne wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.
Kocha Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amefanya mabadiliko ya wachezaji tisa ukilinganisha na kikosi kilichocheza na African Sports katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya Azam Sports Federation Cup.
Kikosi chetu kimepangwa hivi…..
Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Sadio Kanoute (13), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), Moses Phiri (25), Saido Ntibazonkiza (39), Pape Sakho (10).
Wachezaji wa Akiba
Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Kennedy Juma (26), Jonas Mkude (20), Peter Banda (11), Erasto Nyoni (18), John Bocco (22), Jean Baleke (4), Habibu Kyombo (32).