Kikosi kitaka chotuwakilisha dhidi ya Polisi leo

Kocha Mkuu Juma Mgunda, ataanza na washambuliaji wawili katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Polisi Tanzania ambao utapigwa Uwanja wa Ushirika mjini Moshi saa 10 jioni.

Nahodha John Bocco na Moses Phiri wataendelea kuongoza idara ya ushambuliaji ambapo watapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo Clatous Chama na Pape Sakho.

Kiungo mkabaji Sadio Kanoute amerejea kikosini baada ya kuukosa mchezo uliopita na kama kawaida atakuwa sambamba na Mzamiru Yassin.

Kikosi kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Gadiel Michael (2), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Sadio Kanoute (13), Pape Sakho (10), Mzamiru Yassin (19), John Bocco (22), Moses Phiri (25), Clatous Chama (17).

Wachezaji wa Akiba

Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Kennedy Juma (26), Mohamed Ouattara (33), Jonas Mkude (20), Victor Akpan (6), Kibu Denis (38), Habibu Kyombo (32), Jimmyson Mwanuke (21).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER