Kikosi chetu leo saa moja usiku kitashuka katika Uwanja wa Majaliwa kuikabili Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.
Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amefanya mabadiliko ya wachezaji saba ukilinganisha na kikosi kilichocheza mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca mwishoni mwa wiki.
Kikosi kamili kilivyopangwa
Ally Salim (1), Israel Patrick (5), Gadiel Michael (2), Joash Onyango (16), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Pape Sakho (10), Nassor Kapama (35), Jean Baleke (4), Saido Ntibanzonkiza (39), Peter Banda (11).
Wachezaji wa Akiba
Beno Kakolanya (30), Ahmed Teru (31), Jimmyson Mwanuke (21), Ismael Sawadogo (3), Jonas Mkude (20), Habibu Kyombo (32), John Bocco (22), Mohamed Mussa (14), Augustine Okrah (27).