Kikosi Kitakachotuwakilisha dhidi ya Mtibwa

Baada ya kukaa nje kwa takribani mwezi mzima kuuguza jeraha mlinzi wa kulia Shomari Kapombe leo amerejea na ameanza katika kikosi kitakachoshuka dimbani kuikabili Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Kiungo mkabaji Mzamiru Yassin amemaliza adhabu yake ya kutumikia kadi tatu za njano na ataanza pamoja na Jonas Mkude.

Moses Phiri ataendelea kuongoza safu ya ushambuliaji ambapo ataendelea kupata msaada wa karibu kutoka kwa Clatous Chama, Pape Sakho na Augustine Okrah.

Kikosi kamili

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (12), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Pape Sakho (10), Mzamiru Yassin (19), Moses Phiri (25), Clatous Chama (17), Augustine Okrah (27).

Wachezaji wa Akiba

Beno Kakolanya (30), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Mohamed Ouattara (33), Victor Akpan (6), Peter Banda (11), Nassor Kapama (35), Habib Kyombo (32), Kibu Denis (38).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER