Kikosi chetu leo saa 2:15 usiku kitashuka katika Uwanja wa New Amaan Complex kuikabili Mlandege katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi.
Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha amefanya mabadiliko ya wachezaji watatu ukilinganisha na kile kilichoanza kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Singida Fountain.
Benchikha amewaanzisha Ayoub Lakred, Hussein Kazi na Moses Phiri wakichukua nafasi za Ally Salim, Kennedy Juma na Jean Baleke.
Kikosi kamili kilivyopangwa:
Ayoub Lakred (40), Shomari Kapombe (12), Israel Patrick (5), Che malone (20), Hussein Kazi (16), Fabrice Ngoma (6), luis Miquissone (11), Babacar Sarr (33), Moses Phiri (25), Said Ntibazonkiza (10), Willy Onana (7).
Wachezaji wa Akiba:
Ally Salim (1), Hussein Abel (30), David Kameta (3), Kennedy Juma (26), Abdallah Hamisi (13), Ladack Chasambi (36), Salehe Karabaka (23), Jean Baleke (4).