Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya Dodoma Jiji leo

Kocha Mkuu Juma Mgunda na benchi lake la ufundi leo wameamua kuanza na washambuliaji wawili katika mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Mgunda amewapanga pamoja Nahodha John Bocco na Moses Phiri katika safu ya ushambuliaji huku wakipewa msaada wa karibu kutoka kwa Clatous Chama na Kibu Denis.

Mara kadhaa Mgunda amekuwa na utaratibu wa kuanza na mshambuaji mmoja pamoja na viungo washambuliaji watatu lakini leo kaamua kuwapanga Bocco na Phiri kwa pamoja.

Jonas Mkude na Mzamiru Yassin watasimama katika idara ya kiungo wa ulinzi wakati Henock Inonga na Joash Onyango wakisimama kama walinzi wa kati.

Kikosi Kamili kilichopangwa

Aishi Manula (28), Israel Patrick (5), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), John Bocco (22), Moses Phiri (25), Kibu Denis (38).

Wachezaji wa Akiba

Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Mohamed Ouattara (33), Victor Akpan (6),Nassor Kapama (35), Nelson Okwa (8), Habib Kyombo (32).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER