Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya De Agosto leo

Baada ya kukosekana katika mchezo wa ligi uliopita mlinzi wa kati Henock Inonga leo ataanza katika mechi ya hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Premiero De Agosto utakaopigwa saa 12 Uwanja wa Novemba 11.

Katika mtanange dhidi ya Dodoma Jiji, Inonga alipata maumivu wakati wa kupasha misuli kabla ya kuanza mchezo hali iliyosababisha kuwekwa pembeni lakini sasa yuko kamili na ataongoza idara ya ulinzi akiwa na Joash Onyango.

Moses Phiri ataendelea kuongoza idara ya ushambuliaji ambapo atapata msaada wa karibu kutoka kwa Augustine Okrah, Clatous Chama na Kibu Denis.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Israel Patrick (5), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Sadio Kanoute (13), Augustine Okrah (27), Mzamiru Yassin (19), Moses Phiri (25), Clatous Chama (17), Kibu Denis (38).

Wachezaji wa Akiba

Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Jonas Mkude (20), Pape Sakho (10), Nassor Kapama (35), John Bocco (22), Habibu Kyombo (32).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER