Kikosi kitakacho tuwakilisha dhidi ya Wydad

Leo saa 10 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Wydad Casablanca katika mchezo wa Robo Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha Mkuu, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amefanya mabadiliko ya mchezaji mmoja ukilinganisha na kikosi kilichocheza dhidi ya watani Yanga na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 wiki iliyopita.

Kiungo mkabaji, Sadio Kanoute ambaye hakuonekana katika mechi kadhaa zilizopita amerejea kikosini akichukua nafasi ya Erasto Nyoni.

Kikosi kamili kilivyopangwa…..

Ally Salim (1), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Sadio Kanoute (13), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), Jean Baleke (4), Saido Ntibazonkiza (39), Kibu Denis (38).

Wachezaji wa Akiba..

Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Pape Sakho (10), Nassor Kapama (35), John Bocco (22), Moses Phiri (25), Peter Banda (11).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER