Kikosi chetu cha Simba Queens leo saa 11 jioni kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Yanga Princess katika mchezo wa Ligi ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier League – SLWPL).
Kocha Mkuu Charles Lukula amefanya mabadiliko kadhaa ya kikosi kitakachoanza huku akiwaweka benchi baadhi ya nyota ili kuwatumia kipindi cha pili wakihitajika.
Nahodha Opa Clement ataendelea kuongoza mashambulizi akisaidiana na Aisha Juma, Pambani Kuzoya na Jentrix Shikangwa.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
Janeth Shija (30), Daniela Mgoyi (22), Diana Mnali (15), Violeth Nicholas (26), Ruth Ingosi (20), Joelle Bukuru (18), Koku Ally (19), Pambani Kuzoya (17), Aisha Juma (10), Opa Clement (7), Jentrix Shikangwa (25).
Wachezaji wa Akiba
Gelwa Yohan (21), Esther Mayala (23), Dotto Evarist (11), Asha Djafar (24), Vivian Corazone (4), Amina Hemed (14), Philomena Abakah (6), Olaiya Barakat.