Kelvin Ndlomo kocha mpya wa viungo

Uongozi wa klabu umefikia makubaliano ya kumuajiri Kelvin Mandla Ndlomo (30) kuwa kocha mpya wa viungo kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Ndlomo raia wa Afrika Kusini anachukua nafasi ya Sbai Karim raia wa Morocco ambaye mkataba wake ulisitishwa Septemba mwaka huu.

Kabla ya kujiunga nasi, Ndlomo alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Afya na Utimamu wa mwili wa Timu ya Taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ Timu ya Taifa ya Wanawake ‘Banyana Banyana’ Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 na 20 tangu mwaka 2018 hadi sasa.

Ndlomo ana Leseni B ya Ukocha wa Viungo kutoka Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA) aliyoipata nchini Scotland.

KAZI NYINGINE ALIZOFANYA

🔹Mkuu wa Kitengo cha upimaji wa Afya za wachezaji, Mpumalanga Sports and Recreation kazi ya muda (part time) kuanzia mwaka 2021 hadi sasa.

🔹 Mkuu wa Kitengo cha Sayansi ya Afya na Utimamu wa mwili wa timu ya Wanawake; University of Johannesburg (2019-2021).

🔹Mkuu wa Kitengo cha Sayansi ya Afya na Utimamu wa mwili wa timu za Basketball, Rugby na Cricket: St. John College 2018.

🔹 Kocha msaidizi wa viungo wa timu ya wakubwa: Orlando Pirates (2017-2019).

🔹Kocha wa msaidizi wa viungo wa timu ya akiba (reserve team): Kaizer Chiefs (2017 kazi ya muda miezi mitatu).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER