Kauli ya Bocco kabla ya kupaa kwenda Niger

Nahodha wa timu John Bocco amefunguka kuwa mchezo wetu wa pili wa hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Union Sportive Gendarmerie Nationale utakuwa mgumu kuliko wengi wanavyodhani.

Bocco ameyasema hayo leo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kuelekea nchini Niger ambapo kutapigwa mchezo huo Jumapili saa moja usiku.

Bocco amesema licha ya Gendarmerie kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya RS Berkane haimaanishi ni timu mbovu hivyo tutaingia kwa tahadhari kubwa.

“Hatua hii tuliyofikia hakuna mechi rahisi. Gendarmarie imetoka kupoteza mchezo uliopita ugenini hivyo hawatakubali kufanya hivyo tena wakiwa nyumbani.

“Tunaondoka vichwani mwetu tunajua tunaenda kukutana na upinzani mkubwa lakini tumejiandaa kuhakikisha tunapata matokeo mazuri,” amesema Bocco.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER