Kapombe: Tutawashangaza Wydad

Iko wazi kuwa mchezo wetu wa kesho wa Robo Fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca utakuwa mgumu lakini wachezaji wetu wamejipanga kuhakikisha mambo yanakuwa mazuri upande wetu.

Mlinzi wa kulia Shomari Kapombe, amesema wachezaji wamejiandaa kimwili na kiakili kuhakikisha tunapata ushindi mnono nyumbani mbele ya mabingwa hao watetezi wa michuano hii.

Kapombe amesema Wydad ni timu bora lakini tumejiandaa kuhakikisha tunapata ushindi mzuri nyumbani sababu tunajua tukienda kwao Morocco mechi itakuwa ngumu zaidi.

“Tumejiandaa vizuri, tunataka kuwaonyesha Watanzania kuwa tunaweza na tupo tayari. Tumekuwa tukitolewa katika hatua hii lakini sasa tupo tayari kuwaonyesha Watanzania na Wanasimba kuwa tunaweza.

“Tulipoteza nyumbani dhidi ya Raja Casablanca lakini tumekuja na mbinu mpya ambazo tunaamini zitatusaidia. Tunataka kutumia uwanja wa nyumbani kumaliza mechi kwa kuwa tunadhani kule Morocco itakuwa ngumu kwetu,” amesema Kapombe.

Kapombe amewaomba mashabiki wetu kujitojeza kwa wingi uwanjani kwani wana mchango mkubwa katika kufanikisha ushindi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER