Kampeni ya Hamasa kuelekea mchezo dhidi ya Raja yaingia siku ya pili

Leo tumeendelea na kampeni ya kuhamasisha mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani Jumamosi katika mchezo wetu wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca.

Kampeni ya leo imeanzia Makao Makuu ya klabu na kuzunguka mitaa mbalimbali ya Kariakoo, ikaenda Karume na kumalizia soko la Ilala.

Kampeni tuliizindua jana Tegeta katika Tawi la Wazo Hill ambapo tumeendelea na zoezi la kuuza tiketi za mchezo pamoja na jezi.

Muamko wa Wanasimba ni mkubwa wamejitokeza kwa wingi kununua tiketi kwa ajili ya kuipa sapoti timu kwenye mchezo huo mkubwa unaosubiriwa kwa hamu.

Lengo letu ni kuhakikisha tunapambana kwa kila hali ili tuweze kupata ushindi katika Uwanja wa nyumbani.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER