Kakolanya aanza kwa mara ya kwanza NBC

Mlinda mlango Beno Kakolanya ameanza kikosi cha kwanza katika mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Biashara United utakaopigiwa leo saa moja usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa kufuatia Aishi Manula kutokuwa sehemu ya kikosi.

Hii ni mechi ya kwanza ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2021/22 kwa Kakolanya kuanza katika kikosi cha kwanza.

Mbali na Kakolanya nyota wengine ambao wameanza na hakuwepo katika mechi zetu mbili zilizopita za Kombe la Shirikisho Afrika ni Clatous Chama ambaye kanuni zinamzuia na Mzamiru Yassin.

Chama atasaidiana na Pape Sakho pamoja na Peter Banda kumrahisishia kazi Nahodha John Bocco ambaye ataongoza mashambulizi.

Mzamiru atasaidiana na Erasto Nyoni katika kiungo wa ulinzi kuhakikisha wanawalinda vema mabeki watakaokuwa chini ya Henock Inonga na Joash Onyango.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Beno Kakolanya (30), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Erasto Nyoni (18), Peter Banda (11), Mzamiru Yassin (19), John Bocco (22), Clatous Chama (17), Pape Sakho (10)

Wachezaji wa Akiba

Ally Salim (1), Israel Patrick (5), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Bernard Morrison (3), Rally Bwalya (8), Medie Kagere (14), Yusuf Mhilu (27), Jimmyson Mwanuke (21)

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER