Kagere kuongoza mashambulizi dhidi ya Mtibwa leo

Mshambuliaji nyota Medie Kagere amepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa leo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Mara kadhaa Kagere amekuwa akitokea benchi lakini leo Kocha Seleman Matola ameamua kumuanzisha kuongoza mashambulizi.

Kagere atapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Pape Sakho na Peter Banda ambao watatokea pembeni huku Kibu Denis akicheza namba 10.

Mlinda mlango Beno Kakolanya ataendelea kusimama kwenye milingoti mitatu kulifanya lango letu kuwa salama.

Kikosi kamili kilichopangwa

Beno Kakolanya (30), Jimmyson Mwanuke (21), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Pascal Wawa (6), Erasto Nyoni (18), Pape Sakho (10), Sadio Kanoute (13), Medie Kagere (14), Kibu Denis (38), Peter Banda (11).

Wachezaji wa Akiba

Ally Salim (1), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Taddeo Lwanga (4), John Bocco (4), Hassan Mussa (52) , Shafih Hassan( 53), Kassim Omary (55), Yusuf Mhilu (27).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER