Kagere aibeba Simba dakika za jioni

Bao la dakika ya mwisho lililofungwa na mshambuliaji Medie Kagere limetosha kutupa pointi tatu muhimu dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kagere ambaye alitokea benchi alifunga bao hilo kwa kichwa cha chini chini baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Mohamed Hussein kufuatia shambulizi lililoanzia kwa Ibrahim Ajibu.

Dakika 15 za kwanza tulianza kwa kasi kwa kuliandama lango la Namungo na dakika ya tisa almanusura Bernard Morrison atupatie bao baada ya kazi nzuri ya Kibu Denis lakini mpira wake ulitoka pembeni.

Baada ya hapo tuliendelea kutengeneza nafasi huku Namungo wakituacha kucheza wao wakizuia wakiwa wengi langoni kwao.

Dakika ya 51 kiungo mkabaji wa Namungo, Abdulaziz Makame alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea madhambi Shomari Kapombe.

Kocha Hitimana Thierry aliwatoa Morrison, Yusuph Mhilu na John Bocco kuwaingiza Ajibu, Duncan Nyoni na Kagere ambao walionyesha tofauti mchezoni.

Ushindi wa leo unatufanya kufikisha alama 11 baada ya kushuka dimbani mara tano.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER