Inonga, Ntibazonkiza, Kapombe wachuana Mchezaji bora Mei

Nyota watatu wamefanikiwa kuingia fainali ya kinyang’anyiro cha kumtafuta mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi wa Mei (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).

Nyota hao ni mlinzi wa kati, Henock Inonga kiungo mshambuliaji, Said Ntibazonkiza pamoja na mlinzi wa kulia, Shomari Kapombe.

Mechi mbili za mwisho dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union zimechezwa Juni lakini zinahesabika ni za Mei kwakuwa zilizosogezwa mbele kutokana na ushiriki wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Takwimu za wachezaji wote katika mwezi Mei

Dakika Magoli Assisti

Inonga 180 0 0

Ntibazonkiza 450 7 5

Kapombe 360 0 3

Zoezi la kupiga kura limeanza leo kupitia tovuti yetu ya www.simbasc.co.tz na litamalizika Jumatatu saa sita mchana.

Mshindi wa jumla atakabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER