Inonga beki bora Ligi Kuu ya NBC

Mlinzi wetu wa kati Henock Inonga amechaguliwa beki bora wa Ligi Kuu ya NBC 2021/22 katika hafla ya tuzo za TFF zilizotolewa usiku huu.

Inonga amekuwa mhimili muhimu katika idara ya ulinzi ya kikosi chetu na amekuwa na mchango mkubwa kwenye kila mchezo.

Msimu uliopita akiwa na kikosi cha DC Motema Pembe ya DR Congo, Inonga alishinda pia tuzo ya beki bora wa msimu.

Ingawa ni msimu wake wa kwanza Inonga ameonyesha kuimudu vizuri Ligi Kuu ya NBC.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER