Inonga aisaidia DR Congo kutinga robo fainali AFCON

Mlinzi wetu wa kati Henock Inonga ameisaidia timu yake ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutinga robo fainali ya michuano ya AFCON baada ya kuifunga Misri kwa mikwaju ya penati 8-7.

Katika mchezo huo ambao ulimamalizika kwa sare ya kufungana bao moja katika dakika 90 za kawaida Henock akiingia dakika ya 65 kutokea benchi.

Baada ya kuingia Henock alikuwa na mchango mkubwa wa kusaidia timu kuzuia na kushambulia lakini haikuwa rahisi kupata bao la kuongeza.

Henock alipiga penati safi ya tano na kufunga na kusaidia DR Congo kutinga robo fainali ya michuano hiyo.

Henock ndiye mchezaji pekee kati ya sita walioshiriki AFCON kutoka kwenye kikosi chetu ambaye taifa lake limeingia robo fainali hivyo klabu inamtakia kila la kheri.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER