Gomez afurahishwa timu inavyozidi kupaa kwenye msimamo VPL

Kocha Mkuu, Didier Gomez amefurahishwa na hatua ya kuendelea kuweka tofauti kubwa ya alama kwenye msimamo wa Ligi Kuu dhidi ya wanaotufuata ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa msimu huu.

Baada ya mchezo wa jana tumefikisha pointi 61 alama nne juu ya wanaotufuatia huku tukiwa na michezo miwili mkononi kitu ambacho kimemfurahisha Kocha Gomez.

Gomez amesema tumecheza mechi tano ndani ya siku 14 na kufanikiwa kushinda zote hatua iliyotufanya kupanda kileleni mwa msimamo kwa kishindo.

“Ni jambo zuri kuzidi kuongeza tofauti ya alama dhidi ya wanaotufuata katika msimamo, wachezaji wangu wamefanya kazi kubwa hadi kufikia hapa,” amesema Kocha Gomez.

Baada ya mchezo wa jana dhidi ya Dodoma tunajiandaa na mechi ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Jumamosi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER