Gomes: Simba bora si Tanzania tu bali Afrika Mashariki

Kocha Mkuu, Didier Gomes ameweka wazi kuwa msimu huu tumekuwa bora si Tanzania pekee bali Afrika Mashariki nzima na ndiyo maana tumefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu kwa mara ya nne mfululizo.

Gomes amesema kikosi chetu ni bora kulinganisha na vingine ndani ya ukanda huu na ndiyo sababu tumeshinda mechi nyingi pia tumefunga mabao mengi kuliko wote kwa kucheza soka safi.

Aidha, ameupongeza uongozi wa klabu chini ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohamed Dewji ‘Mo’ na Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez kwa kumuwekea mazingira mazuri ya kufanya kazi kwa muda wote tangu atue nchini.

“Simba ni timu bora kwa sasa Afrika Mashariki nzima nadhani baada ya muda tutacheza fainali ya Afrika. Ukiangalia msimu huu tumefunga mabao mengi na tumeshinda mechi nyingi pia,” amesema Gomes.

Gomes amesema ana matumaini ya kufanya vizuri katika mchezo wa Fainali ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

“Dhamira yetu ni kuhakikisha tunachukua na taji la FA na ninatumaini tutafanikisha hilo,” amesema Gomes.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER